top of page

DON BOSCO FEAST 31/01/2021


Don Bosco feast ni sherehe inayo sheherekewa siku ya tarehe 31 mwezi wa kwanza kila mwaka katika kila nyumba ya Don Bosco. Shuleni Don Bosco Didia mwaka 2021 sherehe hiyo iliweza kusherekewa na wanafunzi pamoja na wageni mbalimbali waliweza kufika shuleni hapo Don Bosco Didia wageni hao waliweza kujumuisha kikundi cha wakatoliki kiitwacho VIWAWA ambacho kinajumuisha vijana wakuanzia umri wa miaka kumi nane.Don Bosco ni mtakatifu aliyeweza kuchaguliwa kua msimamizi wa vijana katika jimbo kuu la shinyanga hivyo vijana mbalimbali kutoka sehemu tofauti tofauti za mkoa huo huweza kufika katika shule hii ya Don Bosco Didia ili kuweza kusheherekea siku hiyo.

Sherehe hiyo iliweza kufanyika katika kumbi za shule ya Don Bosco Didia siku hiyo ya jumamosi tarehe 31 ya mwezi wa kwanza mwaka 2021 sherehe ilianza kwa misa takatifu na baadae kufuatiwa na burudani kutoka kwa wanafunzi na vijana wa kikatoliki viwawa ambapo baada ya apo kulikua na speech kutok kwa gombera wa shule hiyo padri Vicent Mokaya na baada ya hapo watu waliweza kwenda kupata chakula cha mchana.Baada ya chakula cha mchana kulifuatiwa na mchezo wa soka kati ya timu ya viwawa pamoja na timu ya vijana wa kidato cha nne wa shule hiyo ya Don Bosco Didiaambayo ilihusisha uzinduzi rasmi wa jezi za vijana hao wa kidato cha nne mtanange huo uliweza kuisha kwa mabao mawili kwa moja ambapo vijana hao wa kidato cha nne waliweza kuibuka videdea kwa magoli mawili yaliyoweza kufungwa na kijana joseph madose pamoja na eubene solomoni wakati goli la upande wa upinzani likifungwa na Joseph Kelvin.Baada ya mchezo huo kuliweza kufuatiwa na rozari ya pamoja ambayo iliongozwa na vijana wa vocation group na baadae watu waliweza kupata chakula cha usiku na kurudi ukumbini kwaajili ya burudani mbalimbali zilizokua zimeandaliawa na baadhi ya vijana ilipofika saa nne na nisu ndipo ilikua tamati ya sherehe hiyo ambayo ilifungwa kwa sala na Baraka kutoka kwa gombera wa shule hiyo padri Vicent Mokaya.


By Don Bosco Didia Young Journalist Club

8 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page