top of page

DIDIA DON BOSCO SEC. YAKICHAKAZA CHUO CHA KOLANDOTO VOLLEYBALL NA BASKETBALL....KOLANDOTO WACHEKELEA


Wachezaji wa Mpira wa Basketball na Volleyball kutoka Shule ya Seokondari ya Don Bosco Didia na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto zote za Shinyanga wakiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya Michezo hiyo kuanza.


Na Josephine Charles- Malunde


Michezo ya Kirafiki kati ya Timu ya wachezaji kutoka Don Bosco Sekondari iliyopo Didia Shinyanga na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho pamoja na uwanja wa Shule ya Msingi Kolandoto imemalizika kwa Don Bosco kuibuka washindi kwenye michezo ya Volleyball na Basketball.


Michezo hiyo ilianza kuchezwa majira ya saa kumi jioni na kumalizika saa moja usiku siku ya Jumamosi ya 20 Feb. 2021 ikihusisha Michezo ya Football,Basketball na Volleyball kutoka Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na Shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo Didia Shinyanga,ambapo katika Mchezo wa Volleyball Don Bosco walishinda Seti 3 kwa 1 dhidi ya Kolandoto,mchezo wa Basketball Don Bosco waliendelea kuongoza kwa kupata alama 57 kwa 30 dhidi ya Kolandoto wakiwa walicheza kota 4.


Hata hivyo Wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa upande wa football walifuta machozi kwa kuwacharaza magoli 4-0 Timu ya Don Bosco Sekondari mtanange uliochezwa katika Uwanja wa shule ya msingi Kolandoto.


Kwa upande wake Mdau wa Michezo na Mratibu wa michezo hiyo ya Kirafiki kati ya Don Bosco Secondari na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Bi. Josephine Charles amewashukuru wachezaji wote kushiriki michezo yote iliyoandaliwa japo kulikuwepo na changamoto ya Mvua pamoja na kuwashukuru wachezaji kutoka Don Bosco Didia kufika Kolandoto kwa ajili ya michezo hiyo na kuwatia moyo wachezaji wote kuzidi kukaza katika michezo na yeye pamoja na wadau wengine wa michezo wapo tayari kuendelea kuwasapoti.


Tazama Picha hapa chini..!!



Huu ni ubao unaoonesha Matokeo ya Mchezo wa Basketball kati ya Don Bosco Sekondari na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.








Wachezaji wa Timu ya Volleyball kutoka chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto ambao walikuwa wenyeji wa mchezo wa Kirafiki wakiwa wamejipanga kupata Picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza.





Wachezaji wa Volleyball kutoka Don Bosco Sekondari ambao walikuwa wageni wa mchezo wa Kirafiki wakiwa wamejipanga kupata Picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza.





Awali akiongea kabla ya michezo yote kuanza katika uwanja wa Basketball Kolandoto mdau wa Michezo na Mratibu wa Michezo hiyo ya Kirafiki kati ya Shule ya Sekondari Don Bosco Didia na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Bi Josephine Charles kutoka Radio Faraja fm stereo 91.3 Shinyanga amewakumbusha wachezaji wote kuwa michezo ni Afya na Burudani hivyo ikitokea Timu fulani imezidiwa nguvu basi wasijenge uhasama bali wafurahi na wajue kuwa wamefanya zoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.



Mdau wa Michezo na Mratibu wa Mechi ya Kirafiki kati ya Don Bosco Sekondari na Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akizungumza na wachezaji kabla ya mechi hiyo kuanza.





Akizungumza baada ya mechi zote kuchezwa Mwenyekiti wa Basketball ya Kolandoto ambaye pia Ni mkuu wa Idara ya Upasuaji kutoka Hospitali ya Kolandoto Kibwana Mgude amewapongeza wachezaji wote walioshinda na walioshindwa katika Michezo yote na kuahidi mechi ya kirafiki Ijayo ambayo wao watasafiri kwenda Didia kucheza na Don Bosco Secondari watahakikisha wanalipa magoli waliyofungwa hasa katika michezo ya Volleyball na Basketball.





Mchezo wa Volleyball ukiendelea uwanjani.








Mashabiki wa Mpira wakiendelea kutazama mechi uwanjani









Mashabiki wa Mpira wakiendelea kutazama mechi uwanjani






53 views0 comments

Recent Posts

See All

コメント


bottom of page