DON BOSCO DIDIA TOURNAMENTS
Don Bosco Didia tournaments ni mashindano yanayofanyika katika shule hii ya Don Bosco Didia kila siku ya ijumaa kwa kila wiki ambapo wanafunzi hua wanashindana katika nyumba(timu) tofautitofauti ambazo hua wana gawanywa katika timu hizo na walimu wa michezo katika shule hiyo ya Don Bosco Didia. Shule hua inanunua jezi za rangi tofautitofauti na kuzigawa kwa wanafunzi ili kutoweza kuleta mchanganyiko wakati wa michezo na pia kuweza kuleta hali ya ushindani katitka timu hizo. Timu hizo kwa ujumla hua zipo nane na zina majina mbalimbali kama vile:Tanganyika,Victoria,manyara,ruaha,ngorongoro,kilmanjaro,meru na Serengeti. Mashindano haya hua yana husisha michezo mbalimbali kama vile mpira wa kikapu,mpira wa miguu,volley ball,mpira wa pete,mpira wa mikono,base ball pamoja na hockey. Mashindano haya hua yana round nne ambazo hujumuisha michezo hiyo yote kwa kila timu kwa timu itakayo shinda kwa moja ya michezo hiyo hupata alama tatu na kwa wae watakao fungwa hupata alama sifuri na wale watako toka sare hupewa alama moja kwa kila timu.